Ligi Kuu

Kamwe: Tumerudi kujipanga

DAR ES SALAAM: MENEJA Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema kikosi hicho kimerudi kambini na kuanza maandalizi ya mchezo wa Dabi dhidi ya Simba, huku akiwatoa hofu mashabiki kuhusu hali ya wachezaji baada ya mapumziko ya ligi.

Kamwe amesema kikosi bado hakijakamilika kutokana na takribani wachezaji 15 kuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa, lakini waliobaki kambini wameendelea na maandalizi.

Amesema wachezaji walioripoti hawana majeraha na wamefika wakiwa katika hali nzuri ya kiafya na kimwili kutokana na programu ya mazoezi waliyopewa wakati wa mapumziko.

“Tumerudi. Tunataka kuwatoa mashaka mashabiki, wanachama na wapenzi wa klabu yetu, hakuna majeraha,” amesema Kamwe.

Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana katika mchezo huo wa Dabi baada ya mapumziko ya ligi yaliyotokana na majukumu ya timu za taifa.

Related Articles

Back to top button