Ariana Grande apumzika shughuli za filamu, muziki

MWIMBAJI maarufu wa Marekani, Ariana Grande, anaendelea kuchukua muda wa kuwa mbali na shughuli nyingi za hadharani, huku akitarajiwa kurejea kwenye majukumu ya burudani baadaye mwaka huu.
Grande alitangaza kuchukua mapumziko baada ya kumaliza ziara yake ya Eternal Sunshine Tour, akisema anahitaji muda wa kujitenga na shughuli za hadharani na kupata nafasi ya kupumzika.
Kwa mujibu wa taarifa mpya, msanii huyo kwa sasa anaendelea na maisha ya kawaida Los Angeles, huku akitumia muda wake nje ya spotlight baada ya miaka kadhaa ya kuwa na ratiba ndefu ya muziki na filamu.
Mapumziko hayo hayamaanishi kwamba Grande ameacha kazi ya muziki na filamu. Anatarajiwa kurejea kwenye shughuli hizoitakapotolewa filamu yake mpya, ‘Focker-In-Law’, inayotarajiwa kutoka Novemba 2026.
Katika filamu hiyo, Grande anacheza nafasi ya Olivia Jones, mpenzi wa Henry Focker, na anaigiza pamoja na mastaa akiwemo Ben Stiller na Robert De Niro.
Taarifa zinaeleza kuwa Grande amepanga kushiriki katika shughuli za kuitangaza filamu hiyo msimu huu, kabla ya kuendelea na kipindi chake cha mapumziko baada ya majukumu hayo.




