Burudani

Zuchu ampigia pande Angella

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Zuhura Othuman ‘Zuchu’ amemuomba boss wake Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumsaini Angella Samson katika lebo ya Wasafi.

Akizungumza wakati anamkabidhi Angella gari kama zawadi, Zuchu amesema atafurahi endapo bosi wake atamsaini kwa kuwa anapambana na muziki.

⁶”Naomba rai kwa bosi wangu ikimpendeza kama alivyowatoa wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Lavalava na D Voice amsaini na Anjella kwa kuwa ni Msanii mzuri na anafanya vizuri.

“Nasema hivyo kwa kuwa naelewa changamoto za kutokuwa kwenye lebo na ilivyokuwa vigumu kutafuta ‘shows’ mbalimbali za kuburudisha, usione msanii anajisifu kuwa analipwa Milioni, sio kitu kidogo kwenye muziki na inahitaji uwekezaji wa hali ya juu.”amesema ‘Zuchu’

Pia ameongeza kuwa amempa zawadi Angella kama sehemu ya kusapoti mwanamke mwenzake katika muziki anaoufanya.

Related Articles

Back to top button