Burudani

Steve humtoi kwenye uchekeshaji

MCHEKESHAJI maarufu nchini Steve Moses ‘Steve Mweusi’ amesema hafikirii kuigiza tofauti na anachokifanya kwa sababu uchekeshaji ni kipaji ambacho kinampa wepesi kwenye kuigiza.

Steve amezungumza na SPOTILEO na kueleza namna anavyofurahia sanaa ya uchekeshaji ambapo amesema kuwa anafurahia zaidi kuliko kufanya sanaa ingine yoyote.

Amesema kitu kingine kinachomfanya aendelee kufurahia ni namna baadhi ya waigizaji wengine wanavyomsaidia kimawazo katika kuhakikisha anapiga hatua kwenye sanaa hiyo.

“Kikubwa wananisisitiza sana kwenye swala la nidhamu  kuwa ndio msingi wa sanaa yetu napia wao wakihitaji msaada wowote kutoka kwangu huwa nashirikiana nao kiukweli na waheshimu na wananionyesha heshima pia,” amesema Steve.

Related Articles

Back to top button