Mastaa

Ciara anatarajia mtoto wa tano

NEW YORK: MWANAMUZIKI Ciara na mumewe, Russell Wilson wametangaza rasmi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa tano.

Wanandoa hao wametangaza taarifa hiyo njema kupitia kurasa zao za Mtandao wa Instagram ambapo waliweka video na picha zinazoonesha tumbo kubwa la Ciara.

Katika picha nyingine Ciara, 40 anaonekana ameanika nguo za watoto wake zenye majina yao na kisha fulana moja ikiwa haina jina na kuandika: “Binadamu mwingine wa kumpenda.”

Kwa pamoja huyo ni mtoto wao wa nne lakini huyo ni mtoto wa tano kwa Ciara kwani awali alipata mtoto wa kiume na rapa Future anayeitwa Future Zahir Wilburn, 12.

Watoto wao wengine wa kike ni Sienna (9), Amora (2) na wa kiume anayeitwa Win (5).

Wawili hao waliofunga ndoa mwaka 2016 ambao mara kadhaa wameeleza kutaka kuwa na familia kubwa, bado hawajataja jina wala siku wanayotarajia kumpata mtoto wao.

Related Articles

Back to top button