Nyumbani
Waamuzi wanne Tanzania kuchezesha CAFCL

DAR ES SALAAM: WAAMUZI wanne kutoka Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya JS Saoura ya Algeria na Horoya AC ya Guinea.
Waamuzi hao ni Nasir Salum, atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Mohamed Mkono na Ally Ramadhani ambao watakuwa waamuzi wasaidizi, wakati Ahmed Arajiga atakuwa mwamuzi wa nne.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Septemba 4, 2026, katika Uwanja wa Miloud Hadefi, Algeria.
Uteuzi huo unaendelea kuonesha kuongezeka kwa imani ya CAF kwa waamuzi kutoka Tanzania katika kusimamia mechi za mashindano ya kimataifa ya ngazi ya klabu barani Afrika.





One Comment