Nyumbani
Fountain Gate ruksa kusajili

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) limeiondolea klabu ya Fountain Gate adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo ya Ligi ya Championship kumlipa madai yake yote Kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman.
“Awali kocha huyo raia wa Misri aliishitaki FIFA klabu hiyo kwa kumvunjia mkataba kinyume cha taratibu,” imesema taarifa TFF.
Kwa hatua hiyo TFF nayo imeiondolea Fountain Gate adhabu ya kufungiwa kusajili.