Muziki

Wimbo wa Nandy, Mbosso na S2Kizzy washika namba 1 YouTube

WASANII wa Bongo Fleva Nandy na Mbosso, wakishirikiana na mtayarishaji S2kizzy, wameendelea kuteka hisia za mashabiki kupitia wimbo wao mpya ‘Malaika’, ambao umeingia katika orodha ya video zinazotrendi Tanzania.

Kwa mujibu wa takwimu za YouTube Trending Tanzania zinazopatikana leo, wimbo wa Malaika umekuwa namba moja kwenye orodha ya video za muziki zinazotrend, huku ukiwapita nyimbo za wasanii wengine akiwemo Rayvanny, Harmonize, Jay Melody na Marioo.

Hali hiyo inaonesha namna muziki wa Bongo Fleva unavyoendelea kupata nguvu kwenye majukwaa ya kidijitali, huku mashabiki wakionesha mwitikio mkubwa kwa kazi mpya za wasanii wa Tanzania.

Kwa upande mwingine, Tanzania imeendelea kuonekana kwenye ramani ya muziki wa Afrika baada ya wasanii 11 wa Tanzania kupata nafasi kwenye uteuzi wa AFRIMMA Awards 2026, ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizoongoza kwa uwakilishi Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button