Mastaa

Mobetto: Miaka mitatu ya ndoa imeniletea baraka na mafanikio

DAR ES SALAAM: MWNAMITINDO na msanii wa filamu, Hamisa Mobetto, amesema miaka mitatu ya ndoa yake na mume wake, Aziz Ki, imekuwa kipindi cha baraka na mafanikio makubwa katika maisha yake.

Hamisa amesema katika kipindi hicho ameshuhudia mabadiliko mbalimbali yenye matokeo chanya katika maisha yake, akiamini kuwa ndoa yake imekuwa sehemu ya baraka na maendeleo anayoyaona kwa sasa.

Akizungumza kuhusu safari hiyo, Hamisa amesema miaka mitatu ya ndoa imempa nafasi ya kuona mafanikio katika maeneo mbalimbali ya maisha yake, huku akieleza kuwa amekuwa akijifunza na kukua katika safari hiyo.

Aidha, mwanamitindo huyo ameeleza namna anavyotumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kushirikisha mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake, akisema matumizi mazuri ya majukwaa hayo yamekuwa yakimfungulia milango ya fursa.

Kwa mujibu wa Hamisa, mitandao ya kijamii imekuwa zaidi ya sehemu ya kushirikisha maisha yake, kwani imekuwa chombo kinachomuwezesha kukutana na fursa mbalimbali za kimaendeleo.

“Miaka mitatu ya ndoa yangu imekuwa na baraka nyingi na mafanikio makubwa.

Pia nimekuwa nikitumia vizuri mitandao ya kijamii kushare mambo mbalimbali ya maisha yangu, jambo ambalo limekuwa likifungua milango ya fursa na maendeleo,” amesema Hamisa.

Kauli hiyo imeendelea kuwavutia mashabiki wake, ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu safari ya maisha ya mwanamitindo huyo pamoja na hatua mbalimbali za mafanikio anayopitia.

Hamisa amekuwa miongoni mwa mastaa wanaotumia mitandao ya kijamii kujenga chapa yake binafsi na kushirikisha shughuli mbalimbali za maisha na kazi zake.

Related Articles

Back to top button