Ligi Kuu

Baraza achekelea kiwango cha Pamba Jiji

DAR ES SALAAM: Kocha wa Pamba Jiji, Fransis Baraza, amesema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake katika mchezo wao dhidi ya Azam FC licha ya kufungwa bao 2-1.

Baraza amesema timu yake ilionesha ushindani mkubwa ndani ya uwanja, huku wachezaji wakionesha nidhamu na kujituma katika kutafuta matokeo chanya.

Amesema licha ya changamoto walizokutana nazo katika mchezo huo, kikosi chake kiliendelea kupambana hadi dakika za mwisho na kuonesha uwezo wa kupigania matokeo.

Kocha huyo amewapongeza wachezaji wake kwa namna walivyotekeleza majukumu yao, akieleza kuwa kiwango hicho kinaonesha timu inaendelea kujenga ushindani.

Baraza amesema bado kuna maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi zaidi, lakini anaamini mwenendo wa timu unaendelea kuwa mzuri na wachezaji watazidi kuimarika katika michezo ijayo.

Amesisitiza kuwa Pamba Jiji itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha kiwango chake na kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika michezo inayofuata.

Related Articles

Back to top button