Muziki

Alikiba, Nandy, Harmonize, Mbosso kukiwasha Kizimkazi Festival

DAR ES SALAAM: WASANII mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva, akiwemo Frida Amani, Alikiba, Nandy, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Mbosso na Omary Mwanga ‘Marioo’, wanatarajiwa kutoa burudani katika Kizimkazi Festival 2026, inayotarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 12 hadi 14, 2026.

Wasanii hao wametangazwa rasmi kuwa sehemu ya burudani katika tamasha hilo, huku mashabiki wakitarajiwa kupata fursa ya kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii wenye mitindo na ladha mbalimbali za muziki.

Kizimkazi Festival inatarajiwa kuwakutanisha Watanzania pamoja na wageni kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kusherehekea, kufurahia burudani na kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana na tamasha hilo.

Mbali na burudani, tamasha hilo linatarajiwa kuwa jukwaa la kuibua na kukuza fursa katika sekta ya utalii, utamaduni na burudani, huku likiendelea kuunganisha muziki na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Ushiriki wa wasanii hao unatarajiwa kuongeza mvuto wa tamasha hilo na kuwapa mashabiki nafasi ya kukutana na burudani kutoka kwa baadhi ya majina makubwa katika tasnia ya muziki nchini.

Related Articles

Back to top button