BurudaniMuziki

Harmonize amuomba Rais Samia kumsaidia Haitham

MSANII wa Bongo fleva Rajabu Abdul, ‘Harmonize’ amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan Kumsaidia matibabu msanii Haitham aliyeko mahututi (ICU)

Akiwa kwenye jukwaa anatumbuiza Harmonize ameomba wamuombee afya njema na matibabu kwa ujumla msanii huyo.

Haitham anasumbuliwa na mapafu hali iliyopelekea kushindwa kupumua kupelekea kulazwa(ICU) katika hospital ya Temeke.

“Kutokana na hali mbaya ya kiafya aliyonayo msanii mwenzetu Haitham tunamuombea kwa Mungu afya njema pia Rais kumsaidia na viongozi wengine mbalimbali katika gharama za matibabu.

“Katika kutambua mchango wa wasanii na yule ni mtoto wa kike alikuwa akipambana kwenye mziki hajafika level ya kujitibu mwenye salamu hizi zimfikie Rais wetu mwingi wa rehema na mwenye upendo.”amesema Harmonize

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button