Kwingineko

Diego Forlan kocha mpya Uruguay

MONTEVIDEO: CHAMA cha Soka cha Uruguay (AUF) kimetangaza Diego Forlan kama kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uruguay.

AUF imefafanua kuwa Forlan atashikilia majukumu ya timu ya taifa na yale ya kikosi cha chini ya miaka 20.

Forlan, 47 amechukua mikoba ya Marcelo Bielsa aliyebwaga manyanga baada ya kushindwa kuondoka na ushindi kwenye mechi zote tatu za Kombe la Dunia 2026.

AUF imeutaja uteuzi wa mchezaji huyo bora wa Kombe la Dunia 2010, amerejea kuonesha ukongwe, ujuzi, uongozi na ubunifu wake katika soka la kimataifa.

Forlan aliyewahi kukipiga Atletico Madrid, Inter Milan na Manchester United aliisaidia Uruguay kutwaa Copa America 2011 kabla ya kustaafu mwaka 2019.

Tangu hapo, amegeukia ukocha na aliwahi kuzinoa klabu za Argentina za Penarol na Atenas huku mechi yake ya kwanza ya kirafiki ya kimataifa ikitarajiwa kati ya Septemba au Novemba, mwaka huu.

 

Related Articles

Back to top button