Burudani

BASATA na CDEA maandalizi creative Economy Expo 2026

DAR ES SALAAM: BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Creative Economy Development Association (CDEA) wameimarisha maandalizi ya Mashariki Creative Economy Expo 2026, maonesho makubwa yatakayowakutanisha wasanii na wadau wa sekta mbalimbali za sanaa na ubunifu kutoka ndani na nje ya nchi.

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga, amekutana na viongozi wa CDEA wakiongozwa na Mkurugenzi wake, Ayeta Anne Wangusa, katika ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia maandalizi ya maonesho hayo.

Kikao hicho kilijikita katika kuweka mikakati ya kuhakikisha Mashariki Creative Economy Expo 2026 inafanyika kwa mafanikio.

Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 18 hadi 21, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

“Maonyesho hayo inalenga kukuza uchumi wa ubunifu, kuongeza thamani ya kazi za wasanii na kufungua fursa zaidi za biashara na ajira kwa wadau wa sekta ya sanaa nchini.

Katika hatua nyingine, BASATA imekutana na mwanzilishi wa Best Barber and Hairstylist Award Tanzania, Edward F. Henry, kujadili maandalizi ya tamasha hilo la mwaka 2026.

Kwa upande wake Henry amewasilisha andiko la tamasha, huku BASATA ikitoa mwongozo kuhusu taratibu na kanuni zinazopaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha tamasha hilo linaandaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia sheria, weledi na viwango vinavyotakiwa katika sekta ya sanaa nchini.

Wataalamu kutoka BASATA pia walishiriki kikao hicho kwa kutoa ushauri wa kitaalamu na kujadili maeneo ya ushirikiano yatakayochochea mafanikio ya Expo hiyo.

Related Articles

Back to top button