Mastaa

Gabo: Nilimfanyia kwa heshima ya Alikiba

....sitacheza tena video za wasanii wa bongo fleva

DAR ES SALAAM: MKALI wa filamu za Bongo Movie, Gabo Zigamba, amesema hataonekana tena katika video za nyimbo za wasanii baada ya kushiriki kwenye video ya wimbo Sumu wa Alikiba akimshirikisha Marioo.

Gabo ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye kipindi cha Crown, alipoulizwa ni utaratibu gani msanii anatakiwa kuufuata ili aweze kushiriki kwenye video ya wimbo wake.

Akijibu swali hilo, Gabo alitumia mfano wa kipekee kueleza msimamo wake.

“Unajua hapa duniani kuna sehemu iliwahi kupigwa na jua mara moja tu, halafu haijawahi kupigwa tena.

Ni ile sehemu ambayo Nabii Musa alipiga fimbo, maji ya bahari yakapasuka. Baada ya maji kurudi katika hali yake ya kawaida, sehemu ile haikuwahi tena kupigwa na jua,” amesema.

Amefafanua kuwa mfano huo unaashiria uamuzi wake wa kushiriki mara moja tu kwenye video ya muziki.

“Nilifanya ile video na sitakuja kufanya video nyingine. Niliifanya kwa sababu ninamheshimu sana Alikiba. Heshima zote ziende kwa King, ninamheshimu Mfalme,” amesema Gabo.

Mashabiki, wamejiuliza huku wengi wakitafsiri kuwa ushiriki wake katika video ya Sumu ulikuwa wa kipekee kutokana na heshima aliyonayo kwa Alikiba.

Related Articles

Back to top button