Michezo Mingine

Kriketi yateua wachezaji 16 Kombe la Dunia

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Kriketi Tanzania (TCA) kimetangaza kikosi cha wachezaji 16 kitakachoiwakilisha nchi katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia hatua muhimu ya mchakato wa kufuzu Kombe la Dunia la Kriketi kwa wanaume.

Michuano hiyo itafanyika Dar es Salaam kuanzia Agosti 8 hadi 18, huku Tanzania ikinufaika na faida ya kucheza nyumbani katika harakati za kusaka alama muhimu kuelekea ndoto ya kufuzu Kombe la Dunia.

Kikosi hicho kitaongozwa na nahodha Kassim Chete, ambaye ataongoza wachezaji waliokabidhiwa jukumu la kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa.

TCA imesema maandalizi ya timu yamekamilika na wachezaji pamoja na benchi la ufundi wako tayari kwa changamoto inayowakabili, huku ikiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao.

Mashindano hayo yajayo yatawakutanisha mataifa yanayowania nafasi ya kuendelea katika hatua zinazofuata za mchakato wa kufuzu Kombe la Dunia, hivyo kila mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wa alama.

Tanzania itaingia kwenye mashindano hayo ikiwa na ari ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wake wa nyumbani na kuendeleza mafanikio ya kriketi ya taifa kwenye jukwaa la kimataifa, huku ikilenga kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mbio za kufuzu Kombe la Dunia.

Related Articles

Back to top button