GolfMichezo Mingine

Gofu kimataifa kufanyika Dodoma

SERIKALI imepanga kujenga uwanja mpya wa kimataifa wa mchezo wa gofu katika eneo la Chamwino jijini Dodoma.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema leo jijini Arusha alipokuwa akifungua Mashindano ya Kimataifa ya Gofu ya NCBA.

Amesema uwanja huo mpya utachangia kuibua vipaji na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.

Mataifa yanayoshiriki michezo ya gofu ya NCBA ni Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Zambia ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa waandaaji zinashindaniwa.

Related Articles

Back to top button