Filamu

David Jonsson atangazwa kuwa Black Panther III

MUIGIZAJI wa filamu, David Jonsson, anayefahamika kupitia filamu za The Long Walk, Rye Lane na Alien, Romulus, ametangazwa kuigiza nafasi ya T’Challa II, mtoto wa marehemu T’Challa, katika filamu ijayo ya Black Panther III.

Tangazo hilo limetolewa na mwongozaji wa filamu hiyo, Ryan Coogler, wakati wa tukio la San Diego Comic-Con 2026, ambapo alimtambulisha rasmi Jonsson kama Black Panther mpya wa kizazi kijacho.

Uamuzi huo unakuja takribani miaka sita baada ya kifo cha mwigizaji Chadwick Boseman, ambaye aliifanya nafasi ya T’Challa/Black Panther kuwa maarufu duniani.

Boseman alifariki dunia mwezi Agosti 2020 baada ya kuugua saratani ya utumbo mpana.

Related Articles

Back to top button