Mastaa

Shamrashamra za 40 ya mtoto wa Wema zimeanza

DAR ES SALAAM: BAADA ya pongezi nyingi kumiminika mitandaoni kufuatia mtoto wa msanii na mfanyabiashara Wema Sepetu na msanii Whozu, Ollie, kutimiza siku 40, maandalizi ya sherehe rasmi yameanza kwa shamrashamra kubwa.

Usiku huo, familia, ndugu na marafiki wamekusanyika nyumbani kwa mama wa Wema Sepetu kwa mkesha maalumu unaotangulia maadhimisho ya Ollie 40.

Shughuli zimeanza kwa hafla ya Henna Night, iliyopambwa na burudani mbalimbali zikiwemo muziki, ngoma na kibao kata, huku wageni wakifurahia mazingira ya upendo, umoja na mshikamano.

Wema Sepetu, akiwa pamoja na mama yake, ameonekana akifurahia maandalizi hayo huku wakipokea wageni mbalimbali waliojitokeza kushiriki shamrashamra hizo.

Mastaa kadhaa kutoka tasnia ya burudani nao wamehudhuria hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa mama wa Wema, jambo lililozidi kuongeza mvuto wa tukio hilo.

Sherehe hiyo ni mwanzo wa maadhimisho makubwa yanayotarajiwa kufanyika kwa ajili ya Ollie 40, huku mashabiki na wadau wa burudani wakisubiri kuona matukio mengine yatakayofuatia katika siku za maadhimisho hayo.

Related Articles

Back to top button