Yanga wameamua ishu ya uwanja wao!

DAR ES SALAAM: RAIS wa Klabu ya Yanga, Hersi Said, ameongoza kikao cha mwisho cha majadiliano kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo.
Kikao hicho kimefanyika leo Mei 12, 2026 jijini Dar es Salaam, kikiwa sehemu ya maandalizi ya kuanza rasmi kwa mradi wa uwanja wa Yanga SC, ambao unatarajiwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa ya miundombinu ya michezo nchini.
Uongozi wa klabu umeeleza kuwa mradi huo unalenga kuimarisha maendeleo ya klabu pamoja na kuongeza uwezo wa miundombinu ya michezo nchini Tanzania.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo, akiwemo mdhamini mkuu Ghalib Said Mohammed, Mtendaji Mkuu wa klabu Andre Mtine, pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji Gerald Kihinga, Makaga na Alex Ngai.
Mradi huo wa uwanja unatarajiwa kubadilisha taswira ya miundombinu ya klabu na kuongeza ushindani katika sekta ya soka nchini.




