Ligi Daraja La Kwanza

Coastal: Kazi ipo kwa Mbeya City ila tutapambana

MANYARA: KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Fikiri Elias amesema wanatarajia mchezo mgumu dhidi ya Mbeya City kesho kutokana na umuhimu wa pointi kwa timu zote mbili katika msimamo wa ligi.

Fikiri amesema Coastal Union ipo nafasi ya 13 huku Mbeya City wakiwa nafasi ya 14, hali inayoufanya mchezo huo kuwa wa ushindani mkubwa kwa kila upande kusaka matokeo mazuri.

“Mchezo utakuwa mgumu kutokana na nafasi ambazo timu zote zipo. Hatuwezi kuingia kwa hofu ya kupoteza, lazima tucheze na kupambana kutafuta matokeo mazuri,” amesema Fikiri.

Kocha huyo ameongeza kuwa licha ya kucheza nyumbani au ugenini, falsafa ya Coastal Union ni kucheza soka la kushambulia huku wakijiandaa kuwadhibiti Mbeya City kulingana na mbinu watakazotumia ndani ya mchezo huo.

“Mbeya City watakuwa tayari kujibu maswali ya Coastal Union, lakini sisi pia tuna mpango wa kuwadhibiti kulingana na watakavyokuja,” amesema.

Related Articles

Back to top button