Afrika Magharibi

Don Jazzy afunguka kuhusu mwanamke anayemtaka:

ABUJA: MTAYARISHAJI wa muziki kutoka Nigeria, Michael Collins Ajereh ‘Don Jazzy’ amefunguka hadharani kuhusu sifa anazozitafuta kwa mwanamke anayetarajia kuwa naye kwenye mahusiano na kutengeneza maisha.

Don Jazzy alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye podikasti ya ‘Is This Seat Taken’ inayoendeshwa na muigizaji Chinasa Anukam.

Katika mazungumzo hayo, Don Jazzy alieleza kuwa anapendelea mwanamke mwenye tabia tulivu na anayefanana naye kwa mtazamo wa maisha.

Alisisitiza kuwa hapendi migogoro wala vurugu katika mahusiano yake.

“Ninapochagua mwanamke wa kutoka naye, kwanza kabisa anatakiwa awe mtu wa kipekee. Pili, anatakiwa awe mpole kwa mwonekano na tabia. Ukianza kunipigia kelele, maana yake unajichumbia mwenyewe. Mimi sipendi stress wala vurugu,” alisema.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 hapo awali aliwahi kueleza kuwa bado hajarejea kwenye uhusiano mpya baada ya kwanza kutoa talaka, akisema kwa sasa anaweka nguvu zaidi katika kuendeleza kazi yake ya muziki.

Related Articles

Back to top button