Mercedes-Benz 560 SEL la Rais Moi kivutio Jamhuri Day

NAIROBI: WAKATI Kenya ikiadhimisha sherehe za Miaka 62 ya Uhuru (Jamhuri Day), gari la kifahari aina ya Mercedes-Benz 560 SEL, iliyokuwa katika utawala wa Rais wa zamani Daniel arap Moi lenye rangi ya bluu iliyong’aa, lilikuwa kivutio kikubwa katika maadhimisho hayo.
Gari hilo limezungushiwa kamba maalumu na kung’aa kana kwamba linamngoja kiongozi, gari hilo lilikuwa kama hazina iliyohifadhiwa kutoka enzi nyingine ya kisiasa nchini Kenya.
Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Kenya ndilo kwa mwaka huu yamefanyika kwa kujikita katika sekta ya utalii ikionesha vitu vyake vya zamani lakini pia wanyamapori na ukuaji wa sekta ya maonesho mbalimbali.
Kwa vijana wengi walioliona kwa mara ya kwanza, gari hilo Mercedes walikubaliana na ukweli kwamba wamejifunza kitu kutokana na gari hilo la kihistoria kwa nchi yao na kiongozi wao Moi.
Francis Waweru kutoka Kumbukumbu ya Rais alisema: “Gari hilo lilitumika kati ya 1991 na 1995. Lote ni ‘custom made’, lisilopenyeka risasi, na limetengenezwa kwa ajili ya VVIP. Limetembea kilomita 21,000 tu, hivyo bado liko katika hali bora sana.”
Waweru amesma gari hilo ni zima linaweza kuendeshwa hadi sasa lakini halitumiki kwa sababu ni gari la maonesho kwa ajili ya urithi wa taifa.
Gari hilo lilitengenezwa maalum nchini Ujerumani kwa oda kutoka Ikulu, aina ya oda ambazo kwa kawaida hutolewa na marais, wafalme au matajiri wakubwa tu.
“Kila rais ana ladha yake. Mercedes ni chapa maarufu kwa magari ya hadhi ya juu ya VVIP,” alisema Waweru katika miaka ya 80 na 90, 560 SEL ilitambuliwa kama mfalme wa magari ya viongozi




