Mastaa
Chino: Nimebarikiwa kupata wazazi wenye upendo

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Isaya Michael Mtambo ‘Chino Kidd’, ameweka wazi jinsi anavyovutiwa na malezi na mwenendo wa wazazi wake ambao wamekuwa mfano bora kwake tangu akiwa mtoto.
Chino amesema kuwa hajawahi kuona wazazi wake wakigombana wala wakinywa pombe, jambo analoliona kama baraka kubwa maishani mwake.
“Tangu nimezaliwa hawajaachana mpaka leo. Nashukuru Mungu kwa kunipa wazazi wakarimu, waliopendana na kuheshimiana. Sijawahi kuona mama yangu na baba yangu wakipigana,” amesema Chino Kidd.
Msanii huyo amesema mfano mzuri wa wazazi wake umemjenga katika maadili na kumfundisha umuhimu wa upendo, heshima na uvumilivu katika familia



