28 waitwa U23 kuikabili Nigeria

WACHEZAJI 28 wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya soka chini ya miaka 23 kitakachoingia kambini Oktoba 13, 2022 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) dhidi ya Nigeria.
Mchezo huo utapgwa Oktoba 22,2022.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Hemed Morocco amewataja magolikipa kuwa ni Aboutwaleeb Mshery, Arjif Amour na Zubery Foba.
Mabeki ni David Kameta, Alphonce Mabula, Pascal Msindo, David Bryson, Haji Mnoga, Abdulrazak Hamza, Twalibu Mohamed, Mukrim Abdallah, Hatibu Kombo, Dickson Mhilu na AbdulMalik Zakaria.
Viungo walioitwa ni Novatus Dismas, Ally Msengi, Edmund John, Tepsi Evance, Abdul Suleiman, Vicent Abubakar, Yusuph Jamal, Mundhir Vuai na Khalid Idd.
Washambuliaji wa kikosi hicho ni Kelvin John, Annuary Jabir, Oscar Paul na Clement Mzize.
Tanzania imefuzu kucheza hatua inayofuata dhidi Nigeria baada ya kuitoa Sudan Kusini.