Mwinyi kutoa mil 1/- kila goli fainali CECAFA U15
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutoa sh milioni 1,000,000 kwa kila goli timu ya taifa ya Zanzibar chini ya miaka 15 ‘Karume Boys’ itakalofunga katika mchezo wa fainali wa CECAFA dhidi ya Uganda Novemba 16.
Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Mohamed Kabwanga imesema shirikisho linamshukuru Rais Dkt Mwinyi kwa mchango wake mkubwa kuendeleza michezo mbalimbali nchini ukiwemo mpira wa miguu.
“Hatua hiyo ya Raisi Dkt, Mwinyi kutoa zawadi hiyo inaonyesha dhamira yake ya kuhamasisha na kutaka maendeleo ya mpira wa miguu Zanzibar,”imesema taarifa hiyo.
Zanzibar imetinga fainali ya CECAFA U15 baada ya kuitoa Sudan Kusini kwa mikwaju ya penalti 4-2 wakati Uganda imeitoa Tanzania kwa mabao 2-1.