Burudani

Mammito amficha mpenzi wake mpya

NAIROBI: MCHEKESHAJI Eunice Wanjiru maarufu kwa jina la Mammito ameweka wazi kwamba anaujauzito na hayupo tayari kumuweka wazi mwanaume wake kwa sasa baada ya kuachana na mchekeshaji mwenzake maarufu Butita.

Mchekeshaji huyo mtarajiwa alifichua kuwa yupo katika uhusiano mpya lakini mwanaume wake haonekani hadharani na watu hawamfahamu licha ya kuwa katika uhusiano kwa miaka minne sasa.

“Hayuko kwenye tasnia ya burudani, na ndivyo nilivyotaka. Baada ya kushindwana na mchekeshaji mwezangu ndani ya tasnia, nilipendelea mtu wa nje ya tasnia niilipenda awe anafanya kitu tofauti na mimi, kitu ambacho sielewi kikamilifu, mradi tu anatusaidia kifedha,” Mammito aliwaambia wandishi wa habari nchini Kenya.

Mamito alificha ujauzito wake hadi mwishoni mwa Oktoba alipofichua habari hizo kwa wafuasi wake zaidi ya milioni moja, ambapo aliwashangaza mashabiki wake kwa tangazo la video.

Licha ya udadisi wa umma kuhusu utambulisho wa baba, Mammito ameendelea kusisitiza usiri wake kwa mpenzi wake huyo mpya aliyempa ujauziti kwa sababu wanasafari ndefu ya maisha na hataki afahamike mitandaoni.

Katika mahojiano hayo, Mammito alieleza kuwa anapendelea kumweka mpenzi wake asionekane na watu ili kuepusha uchunguzi usio wa lazima.

“Nitamweka faragha kwa sababu huko Nairobi, huwezi kujua. Unamweka hadharani watu wanaanza kumkosoa wakisema, ‘Oh, haonekani mzuri,’ au wengine hata kujaribu kumwibia,” amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 31.

Related Articles

Back to top button