Nyumbani

“Kimataifa,Tanzania,hakuna wa kuisumbua Yanga” – Aziz Ki

DAR ES SALAAM. KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki amekiangalia kikosi cha timu hiyo na kudai kwa sasa kipaumbele chao ni kutafuta kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Akizungumza na Spotileo leo,  Aziz Ki amesema wamefanya vizuri katika mashindano ya ndani na sasa wanatakiwa kupambana na kuongeza nguvu zaidi katika michuano ya Kimataifa ikiwemo kucheza fainali ya Afrika

Amesema kwa misimu miwili aliyocheza Yanga na kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho kwa kuchukuwa mataji yote ya ndani na kuifunga kila timu katika ligi kuu.

“Kwa sasa kipaumbele chetu ni ligi ya Mabingwa kucheza fainali, ligi ya ndani hakuna mpinzani,  nilikuwa sahihi kumuamini Rais Hersi Said kwa miaka hii miwili  ya ajabu , Asante kwake sasa tusonge kileleni mwa Afrika.

Ndio kipaumbele chetu na kila kitu kipo mikononi mwake , anaweza kufanya kitu na kufikia malengo hayo, tuliahidiana tangu mwanzoni nasaini kuitumikia Yanga,” amesema nyota huyo.

Amesema kwa sasa viongozi wanatakiwa kufikiria na kuwekeza zaidi katika michuano ya Afrika, kwa kusonga mbele zaidi kucheza nusu hadi fainali ya michuano hiyo ambayo msimu huu wamefikia hatua ya robo kwa kuwa ndani tayari wamefanikiwa sehemu kubwa.

Aziz Ki ameonyesha kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga kwa kusaidia timu hiyo kufanikiwa kucheza kombe la Shirikisho la Afrika msimu 2022/23 na kuipeleka timu hiyo makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25.

Kiungo huyo kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya wa kutimikia timu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button