FA

Yanga yasanuka mitego

DAR ES SALAAM: KUELEKEA mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Coastal Union, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa timu yao inaingia uwanjani kwa tahadhari na umakini mkubwa ili kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Kamwe, hivi karibuni kumekuwa na matokeo ya kushtua katika mashindano haya, hali ambayo Yanga haitaki kujikuta nayo. Hivyo, wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanakwepa mtego wa kushindwa kusonga mbele.

“Wachezaji wetu wana morali ya juu sana, tunaingia katika mchezo huu kwa umakini wa hali ya juu kwa sababu tunakutana na mpinzani mwenye uzoefu mkubwa, Coastal Union ni timu kongwe inayojua presha ya mashindano kama haya, kwa kuwa mechi hii ni ya mtoano, tunapaswa kushinda ili kuendelea na safari yetu,” amesema .

Aidha, Kamwe amesisitiza kuwa matokeo ya hivi karibuni, ambapo timu kama Azam FC iliondolewa kwenye mashindano, yamezidi kuwaamsha Yanga kuhakikisha hawafanyi makosa.

Kwa kuzingatia changamoto hizo, Yanga imejipanga ipasavyo kuhakikisha inapata matokeo mazuri na kusonga mbele.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button