Ligi Kuu

Yanga yaiwekea mtego KMC

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema wako vizuri na wana motisha ya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC, kesho Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi.

Amesema KMC FC inapenda kucheza soka safi kama ilivyo Yanga na wanatarajia kuwa na moja ya mechi nzuri sana na yenye ushindani mkubwa.

“Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi kwakuwa wenzetu nao watafanya jitihada ili wapate ushindi lakini tupo hapa kwaajili ya kupambana na tunaamini tutawaheshimu na tutafanya vizuri” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa mara zote yaliyopita huwa yamepita, kila mechi huja tofauti, msimu uliopita walicheza nao Chamazi na Morogoro utakuwa mchezo tofauti japo kuwa wana uzoefu wa kucheza nao.

“Kwangu napenda kufunga mabao mengi na kutengeneza nafasi nyingi lakini sote tunatambua kuwa jambo la muhimu kabisa kabisa kesho ni kupata alama tatu,” amesema Gamondi.

Naye Mwakilishi wa wachezaji wa Yanga, Denis Nkane amesema maandalizi waliyofanya yanawapa nguvu na imani ya kushinda mchezo wa kesho dhidi ya KMC FC na wanatarajia kukutana na ushindani mkubwa.

“Kikubwa wachezaji tunatambua umuhimu wa pointi tatu, kitu cha kwanza tunachokiwaza ni ushindi bila kujali idadi ya mabao, tuna morali ya kuwafurahisha hapo kesho,” amesema Nkane

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button