Africa
Yanga, Simba vitani CAFCL
TIMU za Yanga na Simba zinashuka kwenye viwanja tofauti ugenini leo katika michezo ya kwanza ya raundi ya awali kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu ya Wananchi, Yanga itakuwa mgeni wa Al-Merrikh ya Sudan kwenye uwanja wa Uwanja wa Pele Kigali, Rwanda.
Wekundi wa Msimbazi, Simba itakuwa mgeni wa Power Dynamos ya Zambia kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo jiji la Ndola.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga na Simba wameambatana za klabu hizo kama sehemu ya hamasa kwa wachezaji wa timu zao.