Africa
Jwaneng Galaxy kuitibulia Simba leo?
KLABU ya Simba leo inashuka dimbani Dar es Salaam kuikabili Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) hatua ya makundi.
Katika mchezo huo wa kundi B utakaofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba inahitaji ushindi wa angalau bao 1 tu kufuzu robo fainali.
Mchezo mwingine wa kundi hilo leo Wydad Casablanca ya Morocco itakuwa mwenyeji wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwenye uwanja wa Marrakesh uliopo jiji la Marrakesh.
Msimamo wa kundi B kabla ya mchezo wa leo ni kama ifuatavyo:
# | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | 5 | 3 | 2 | 0 | 7 | 1 | 6 | 11 | |
2 | 5 | 1 | 3 | 1 | 3 | 2 | 1 | 6 | |
3 | 5 | 2 | 0 | 3 | 2 | 4 | -2 | 6 | |
4 | 5 | 1 | 1 | 3 | 1 | 6 | -5 | 4 |
Mechi za makundi meingine ni kama ifuatavyo:
KUNDI A
Mamelodi Sundowns vs TP Mazembe
Pyramids vs FC Nouadhibou
KUNDI C
Esperance vs Al Hilal Omdurman
Petro Atletico vs Etoile du Sahel