Yanga na Kagoma daima dam dam

DAR ES SALAAM: MWANASHERIA wa Yanga, Patrick Simon amesema kiungo Yusuph Kagoma ni mali ya klabu hiyo na alisaini mkataba wa miaka mitatu machi 2024 na kwamba Wananchi waliilipa Singida Fountaini Gate ada ya uhamisho Tsh. Million 30 kwa ajili ya mchezaji huyo.
Simon amesema kuwa Machi 4, kamati ya utendaji ya Yanga ilianza mazungumzo na Singida Fountain Gate juu ya Kagoma na uongozi huo wa timu hiyo, ulitoa sharti kwa wananchi kuwa ili kupata huduma ya kiungo huyo basi walipe kiasi hicho cha fedha.
Ameeleza kuwa Klabu hizo mbili ziliingia kwenye makubaliano ya mkataba uliosainiwa na pande zote mbili huku mkataba ukitaka fedha zilipwe kwa awamu mbili yaani Mil 15 na mwisho wa Juni kumalizia 15 zilizobakia.
Mwanasheria huyo amesema Aprili 30, Yanga iliingiza Mill 30 zote kwa timu kwa mujibu wa mkataba wakawa tayari Kagoma, mchezaji halali wa Yanga, June 6, walipokea barua kutoka Singida Fountain Gate kuomba yale malipo ya fedha hizo yawe ya Nickson Kibabage ambaye alikuwa kwa mkopo.
“Yanga hatukujibu barua lakini Julai, 6 tuliwaingizia mill 30 ya mchezaji kwani bado tulikuwa hatujawapa fedha yao na tulijua tu labda wana matatizo ya kifedha, Septemba 5, Kagoma na wanaomsimamia walikuja Yanga na kutuomba tumalize hizi tofauti mezani lakini hakuna kilichoendelea,” amesema Mwanasheria huyo wa Yanga.
Amesema mchezaji amekosea na wanachokitaka nyota aje hadharani na kuomba msamaha hizo pesa waliyomsajili sio yake wala Rais wa Yanga, Hersi Saidi, fedha za wanachama wetu waliojisajili je wananchi wataachaje hela yao iende bure?
“Kilichopo ni kwamba Kagoma anacheza huku akiwa na mkataba wa timu mbili, Yanga tulienda kwenye Kamati ili kumsaidia nyota avunje mkataba mmoja na abaki na mkataba halali,
Kanuni ambazo zinatuongozwa tunataka kuona kanuni hizo zikitenda hali maana mwanzo kwenye shauri mchezaji aliambiwa asitumike ila kafanya hivyo na kwa sasa anahesabika kama mchezi mwenye mkataba wat imu mbili.
Amesema kanuni zinasema kuwa mchezaji inabidi afungiwe lakini wanashangaa kwanini anacheza wakati mwenyekiti wa Kamati ya alishatoa maagizo mchezaji asitumike mpaka shauri litakapomalizika.