Filamu

Wolper: Msiwachukulie poa beki 3

DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu nchini, Jacqueline Wolper ameshauri wanawake kuwapenda na kushirikiana na wadada wanao wasaidia kazi pamoja kulea watoto wao nyumbani .

Wolper amesema wadada wa kazi nao wana uwezo mzuri na ushauri katika mambo mbalimbali ameeleza kuwa wazo lake la kujenga nyumba lilitoka kwa msichana wake wa kazi.

“Mimi wazo la kujenga nyumba nililipata kwa dada wa kazi (house girl) wangu, nilikuwa namlipa mshahara kumbe alikuwa anatunza hadi siku aliyokuja kuniambia anashukuru kwa pesa nilizokuwa nikimlipa.

“Dada nashukuru kwa msaada wako mimi nimejenga nyumba kupitia mshahara wako” Hapo ndipo akili ikanijia kuwa kumbe hata mimi naweza kujenga nyumba kwa kutunza pesa kidogo kidogo”

“Tangu hapo nilianza kutunza pesa kwa ajili ya nyumba na hatimaye nikafanikiwa kujenga nyumba kubwa, nzuri ambayo thamani yake huenda ni zaidi ya Sh milioni 500 ingawa bado haijaisha vizuri.”

Related Articles

Back to top button