Wolfsburg yamnasa Eriksen

WOLFSBURG: KLABU ya Bundesliga ya VFL Wolfsburg imetangaza kumsajili Mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, alikua mchezaji huru tangu mkataba wake na Manchester United ulipomalizika mwishoni mwa mwezi juni mwaka 2025 akifanya mazoezi binafsi kujiimarisha na Klabu ya Molmo ya Sweeden.
“Wolfsburg ni klabu yangu ya kwanza kwenye Bundesliga, kwakweli nimefurahi sana kuanza maisha mapya hapa. Nina hakika tunaweza kupata kitu hapa Wolfsburg pamoja. Mazungumzo na wakuu wa klabu yameenda vizuri sana.” – Eriksen alinukuliwa katika taarifa ya Klabu.
Eriksen ni mchezaji mzoefu, amecheza mechi 310 kwenye Premier League na Tottenham kati ya 2013 na 2020. Pia amechezea Ajax, Brentford na Inter Milan huku uongozi wa Wolfsburg ukiamini uzoefu na ubora wa kiungo huyo katika mafanikio yao.
Eriksen alianguka wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Euro 2020 iliyopigwa 2021 dhidi ya Finland katika uwanja wa Parken Stadium jijini Copenhagen Uholanzi. Alipatiwa huduma ya haraka ya kifaa cha ‘defibrillator’. Baadaye, aliwekewa kifaa cha kupandikizwa ili kufuatilia mapigo ya moyo wake. Amefunga mabao 46 katika mechi 144 za kimataifa.