EPL

White asaini miaka minne Arsenal

Beki wa Arsenal, Ben White amesaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu hiyo.

White, 26, alijiunga na ‘The Gunners’ kwa ada ya £50m mwaka 2021 na ni sehemu muhimu ya kikosi cha Mikel Arteta, akicheza nafasi ya beki wa kulia na kati.

Muingereza huyo alicheza juzi Arsenal ilipotinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 kwa kuifunga Porto.

Tangu ajiunge akitokea Brighton, amecheza mechi 97 za Premier League, akifunga mabao manne.

Amecheza mechi 27 kwenye ligi kwa upande wa Arteta msimu huu huku The Gunners wakiwa kileleni mwa msimamo wa EPL juu ya Liverpool kwa tofauti ya mabao.

Related Articles

Back to top button