Nyumbani

Waziri Mwigulu amkingia kifua Mzize

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kulingana na ubora walionyesha mshambuliaji wa Taifa Stars, Clemente Mzize anatakiwa kupongezwa, sio kukatishwa tamaa.

Kauli hiyo Waziri huyo inakuja baada ya Taifa stars kupoteza mchezo wake wa awali ugenini kwa bao 1-0 la kujifunga la mshambuliaji Clement Mzize mchezo uliopigwa kwenye dimba la Martyrs, Kinshasa DR Congo

“Nimeona maneno kuhusu Mzize, kwangu tumejifunga kwa sababu tumeshambuliwa, tumejifunga kwa kuwa tumeshambuliwa, nyota huyo amejifunga kwa sababu alikuwa mahali pakuzui. Kwangu mimi Mzize anatakiwa kupongezwa kwa kuwa mshambuliaji alierudi kuzuia,” ameandika Waziri huyo katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

Kikosi cha Taifa Stars tayari kimerejea nchini na kuendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa marudiano, Jumanne Oktoba 15 Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button