Burudani

‘Wasanii fanyeni haya mtakua salama’

DAR ES SALAAM: Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kedmon Mapana, amewataka wasanii kuzingatia maadili katika kazi zao za sanaa ili kujijengea heshima ndani ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa maadili kwa waandishi wa habari na wasanii, Mapana alisema kuwa kufuata maadili katika sanaa kunaleta heshima kwa msanii binafsi na jamii kwa ujumla.

“Tumepata nafasi ya kukaa na wasanii pamoja na waandishi wa habari ili kuwapa mwongozo kuhusu maadili, kwa lengo la kuhakikisha kuwa hawarudii makosa katika kazi zao za sanaa,” amesema Mapana.

Kwa upande wake, msanii Blandina Chengula, maarufu kama ‘Johari’, aliwasisitiza wasanii, hasa wanawake, kujiheshimu na kuepuka kutegemea uzuri wao kama njia ya kupata nafasi kwenye tasnia ya filamu.

“Wanawake na wasichana wanapaswa kuhakikisha wanafanya sanaa kwa kutegemea vipaji vyao, badala ya kutumia urembo au mahusiano ya kimapenzi kupata nafasi. Mwisho wa siku, utajikuta umefanya kazi moja au mbili tu, kisha safari yako inaishia hapo,” amesema Johari.

Ameongeza kuwa msanii anatakiwa kutofautisha maisha yake binafsi na maisha ya kazi ili kujijengea thamani kubwa zaidi katika tasnia ya sanaa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button