Muziki

Wanawake watalawa tuzo za MTV Ulaya

Taylor Swift azoa nne

MANCHESTER: MWANAMUZIKI tajiri zaidi kwa wanawake duniani, Taylor Swift ameongoza katika Tuzo za Muziki za MTV Ulaya 2024 zilizofanyika huko Manchester nchini Uingereza usiku wa Jumapili.

Usiku huo wa tuzo ulitawaliwa na wasanii wa kike akiwemo Tyla na Sabrina Carpenter.

Katika sherehe hizo wasanii wenye majina makubwa katika muziki walishindanishwa na Taylor Swift akaibuka na tuzo nne ikiwemo Msanii Bora, Msanii Bora wa Live, Msanii bora wa Marekani na Video Bora ya wimbo wake wa ‘Fortnight’ alioshirikiana na Post Malone.
Hata hivyo mshindi huyo wa tuzo nne hakufika kupokea tuzo hizo lakini katika ujumbe wake uliorekodiwa kabla, Swift ameeleza masikitiko yake kwa kushindwa kuhudhuria tukio hilo huku akieleza kuziamini tuzo hizo.

Washindi wengine walioshinda tuzo nyingi ni Tyla aliyeshinda tuzo tatu, ukiwemo wimbo bora wa R&B wakati Carpenter ameshinda tuzo ya wimbo bora na wimbo wake wa ‘Espresso’.

Swift, ambaye ziara yake ya ‘Eras’ inayoendelea ndiyo yenye faida kubwa zaidi katika historia ya muziki wake aliteuliwa katika vipengele saba kutokana na mwaka huu kutoa albamu yake ya 11 ya the ‘The Tortured Poets Department’.

Mwanamuziki Beyonce ambaye ni mke wa rapa Jay-Z ndiye aliyeibuka na tuzo ya msanii bora na kuwazidi, Billie Eilish na Post Malone pamoja na nyota wa Uingereza Raye, ambaye alishinda tuzo sita katika tuzo za Brit za mwaka huu.

Kama ilivyo kwa tuzo za Grammy za tasnia ya muziki nchini Marekani, wasanii wa Latino, wakiwemo nyota kama vile Puerto Rican Bad Bunny na Karol G wa Colombia waliachwa nje ya makundi ya juu mwaka huu licha ya vibao vyao vya kimataifa.

Tuzo pekee ya mwanamuziki aliyeweka alama kubwa katika muziki kimataifa imekwenda kwa rapa Busta Rhymes.

Hii ilikuwa tuzo za kwanza za MTV Europe tangu mwaka 2022 baada ya vita kati ya Israeli na Hamas kuhairisha tuzo hizo mwaka jana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button