Varane akubali yaishe
BEKI wa zamani wa Real Madrid, Manchester City na timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 31
Uamuzi huo ambao umeshtua wengi umetangazwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambako beki huyo ameandika
“Wanasema vitu vizuri lazima vina mwisho. Katika ‘career’ yangu nimepitia changamoto nyingi sana, tukio baada ya tukio mengi yalikuwa kama hayawezekani hisia na kumbukumbu ambazo nitabaki nazo maisha yangu yote. Kwa tafakuri hii ni kwa fahari kubwa natangaza kustaafu mchezo ambao wote tunapenda” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
“Katika kipindi chote hiki nimepambana kwa taifa langu, klabu zangu, wachezaji wenzangu na mashabiki wa kila timu niliyoichezea nimefurahia kila dakika ya kila mchezo” imeendelea taarifa hiyo
Ikumbukwe kuwa Varane alijiunga na klabu ya Como inayoshiriki ligi ya Italy Serie A baada ya mkataba wake na mashetani wekundu Manchester united kumalizika mwisho wa msimu.
Alisaini mkataba wa miaka miwili lakini alipata majeraha makubwa dakika 23 tu za mchezo wake wa kwanza wa klabu yake mpya dhidi ya Samprodia kwenye Coppa Italia mwezi uliopita.
Varane aliyetokea katika academy ya klabu ya Lens ya ligi kuu ya Ufaransa ameshinda karibu kila taji katika maisha yake ya soka ikiwemo Kombe la dunia, Ligi ya mabingwa barani Ulaya, Laliga, Kombe la FA England, Carabao Cup, Copa del Rey na mengine mengi.