Kwingineko

Mtayarishaji wa Jay-Z, Jennifer Lopez,afariki dunia

NEW YORK: MWANZILISHI mwenza na mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya The Murder Inc, Irv Gotti amefariki dunia akiwa na miaka 54.

Kulingana na The Hollywood Reporter iliyothibitisha kifo chake imeeleza kwamba chanzo cha kifo cha mwanzilishi huyo bado haijajulikana.

Irv ambaye amefanya kazi na wasanii maarufu akiwemo Jay-Z, Jennifer Lopez, Ja Rule, Ashanti na DMX alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi na kisukari kuanzia mapema mwaka jana.

Kufuatia habari hizo za kusikitisha, kampuni ya Def Jam imeeleza:
“Michango yake kwa Def Jam, kama mkurugenzi mkuu na kwa ushirikiano na Murder Inc, ulisaidia kufungua njia kwa kizazi kijacho cha wasanii na watayarishaji, nguvu ambayo ilibadilisha sura ya muziki wa hip-hop na R& B. Ustadi wake katika ubunifu kulizalisha vibao vingi vya wasanii maarufu.

Pia wasanii kadhaa akiwemo Kanye West wametoa salamu zao za pole kutokana na kifo cha mtayarishaji huyo kwa kuweka emoji ya njiwa mweupe kwenye kurasa wake wa Instagram.

Naye 50 Cent katika kumuenzi Irv, ameweka picha yake akiwa anavuta sigara karibu na jiwe la kaburi lililoandikwa ‘RIP’ kisha akaandika: “I’m smoking on dat Gotti pack, nah God bless him’’, kisha akaweka emoji ya njiwa mweupe.

Nyota huyo alifanya kazi katika studio ya Def Jam, ambapo alikuwa kichocheo katika muziki na kazi za Jay-Z, Ja Rule na DMX.

Murder Inc ilizinduliwa katika Jiji la New York mwaka 1998, na baadaye aliandaa albamu ya Vanessa Carlton ya 2007 ‘Heroes and Thieves’ pia aliandaa albamu ya Rick Rubin na Stephan Jenkins.

Related Articles

Back to top button