Ademola Lookman: Shujaa wa Afrika
Ademola Lookman ameandika jina lake katika vitabu vya kihistoria baada ya kutupia mabao matatu dhidi ya Bayer Leverkusen katika usiku mkubwa wa fainali ya ligi ya Europa.
Mabao hayo matatu(Hat- trick) yamemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat-trick katika hatua ya fainali ya michuano hiyo.
Lookman,ambaye ni mchezaji kutoka Naijeria,aliwahi pia kuitumikia klabu ya Everton na RB Leipzig, kisha kutumikia kwa mkopo vilabu vya Fulham na Leicester City. Lakini licha ya kutopata mafanikio kama mchezaji binafsi katika vilabu hivyo,sasa atabaki kuwa shujaa wa kudumu katika historia ya klabu ya Atalanta baada ya kusitisha rekodi ya Bayer Leverkusen ya kutopoteza michezo 51 iliyopita.
Ubungwa huu ni wa kwanza Kwa Atalanta tangu mwaka 1963 na ni ubingwa wa pili katika mshindano makubwa katika historia ya timu hiyo.
Hakika Lookman ni shujaa wa Atalanta; ameipa heshima nchi yake ya Naijeria,na Afrika kwa ujumla!