Mastaa

Ukweli wa Mahusiano ya Millard Ayo na Meena Ally

DAR ES SALAAM:MTANGAZAJI maarufu wa Tanzania, Millard Ayo, amekanusha uvumi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji mwenzake, Meena Ally.

Millard ameeleza kuwa Meena ni mfanyakazi mwenzake na rafiki ambaye anamchukulia kama dada yake, na kwamba ushirikiano wao wa karibu kazini umesababisha watu wengine kudhani vinginevyo.

Amesisitiza kuwa anapokuwa kwenye mahusiano, hupenda kuweka mambo yake binafsi faragha na hajawahi kuwa na mwenza anayependa kuweka mahusiano yao hadharani.

Kumekuwa na mijadala kuhusu ukaribu kati ya Millard na Meena, hasa baada ya Meena kumwandikia Millard ujumbe wa kumtakia heri ya kuzaliwa uliojaa maneno ya upendo na urafiki, hali iliyozua maswali kutoka kwa wafuasi wao kuhusu aina ya uhusiano wao.

Related Articles

Back to top button