Burudani

Tuzo za Kitaifa za Sanaa 2025 Zimbabwe zapamba moto

HARARE: MAJINA ya wawania Tuzo za Kitaifa za 2025 (NAMAs) yamewekwa wazi huku ukitarajiwa ushindani wa hali ya juu katika muziki nchini Zimbabwe.

Katika tuzo hizo kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kike, Shashl, anayejulikana kwa sauti yake ya kipekee katika uimbaji, atachuana na Janet Manyowa na mwigizaji maarufu Tamy Moyo huku kwa wananmuziki wa kiume hali ikiwa ya ushindani zaidi.

Kwa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Mafanikio, ambayo zamani ilijulikana kama Mwanamuziki Bora Anayefanya vizuri ambapo nyota watatu wanaochipukia wanachuana akiwemo Nisha Ts, mwana hip hop Young Gemini na mkali wa Dancehall, Chillmaster anakamilisha orodha hiyo na kuifanya kivutio kwa mashabiki wa muziki nchini humo kutaka kujua nani ataibuka kidedea.

Kwenye tuzo ya Kikundi cha Muziki Bora zaidia vipo vikundi vitatu vya nyimbo za injili vikipambana, huku Joyfull Praise, Shower Power, na The Unveiled zote zikishindania kwa tuzo kuu.

Maonesho yao ya hali ya juu na albamu bora zaidi katika mwaka uliopita zimeimarisha nafasi zao kama baadhi ya vikundi vya muziki vinavyopendwa zaidi nchini humo.

Kipengele cha Wimbo Bora zaidi kinaangazia nyimbo zilizofanya vizuri mwaka 2024, ukiwemo ‘Madiro’ na Kae Chaps, ‘Kana Ndanyura’ wa Killer T, ‘Gore Rino’ wa Tembalami akiwa na The Unveiled, ‘Denga’ wa Hwinza, na ‘Gore Remix’.

Tuzo nyingine zinazogombewa ni Albamu Bora ya mwaka, Ubunifu na thamani ya juu ya utayarishaji, Tuzo la Chaguo la Watu linalotarajiwa huangazia safu iliyojaa nyota, na kuwaruhusu mashabiki kutoa maoni yao kuhusu ni nani atatwaa tuzo hiyo.

Related Articles

Back to top button