Tetesi
Timo Werner kurejea EPL

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea Timo Werner anatarajiwa kurejea Ligi Kuu England(EPL) Januari 2024 baada ya RB Leipzig kutangaza kwamba ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo majira ya baridi.
Baada ya kung’ara Leipzig kipindi cha mwanzo katika klabu hiyo, Werner alihamia Stamford Bridge mwaka 2020 kwa da ya pauni milioni 47.
Hata hivyo, alivumilia wakati mgumu London Magharibi, akifunga mabao 10 tu katika mechi 56 za EPL na baadaye kurudi tena Leipzig.