Tetesi za uhamisho wa soka

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameweka wazi kwamba atakuwa tayari kujiunga na Chelsea majira haya ya joto lakini kwa msimu mmoja tu akionekana bado lengo lake ni uhamisho huru kwenda Real Madrid mwaka 2024.(Sport).
Kuchukua nafasi ya Mbappe, PSG wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Benfica, Goncalo Ramos ambaye ataigharimu miamba hiyo ya Ufaransa pauni milioni 70 sawa na shilingi bilioni 212.8.(A Bola)
Ousmane Dembele pia tajiunga na PSG kutoka Barcelona ambayo haitasajili mbadala wa moja kwa moja na badala yake kuweka imani kwa kinda Ansu Fati.(Sport)
Harry Kane atakuwa tayari kusaini mkataba mpya Tottenahm Hotspur iwapo klabu hiyo itaonesha maendeleo makubwa chini ya Kocha mpya, Ange Postecoglou. (Evening Standard)
Spurs inakabiliwa na ushindani kutoka Al Nassr ya Saudi Arabia kuhusu usajili wa beki wa kati Clement Lengle, ambaye anaweza kuhamia Mashariki ya Kati kwa pauni milioni 13 sawa na shilingi bilioni 39.5 akitokea Barcelona.(Sport)
Majaribio ya Manchester City kumpa mkataba mpya Kyle Walker yamekwama, huku nia ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England ni kujiunga na Bayern Munich majira haya ya joto.(The Athletic)
Chelsea inakabiliwa na ushindani kumsajili kiungo wa Brighton & Hove Albion, Moises Caicedo baada ya ombi la timu isiyojulikana kukataliwa linalozidi ofa ya hivi karibuni ya The Blues ya pauni milioni 80.(Athletic)
Klabu hiyo isiyojulikana ni Liverpool, ambayo ina nia kutafuta kiungo mpya. (Football Insider)
Manchester United sasa imejiunga na Liverpool kumfuatilia kiungo wa Southampton Romeo Lavia.(Independent)
Mazungumzo pia yameimarishwa kati ya Man Utd na kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, ambaye anataka kubaki kwa mabingwa hao wa Bundesliga.(Sky Sports)
Tottenham inakaribia kufikia dili kumsajili mshambuliaji wa Rosario Central, Alejo Veliz, ambaye anatarajiwa kuuzwa kwa kipengele cha kuachiwa cha zaidi ya pauni milioni 13.(German Garcia Grova)
Inter Milan imeelezea nia ya kumsajili beki wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu.(Gazzetta dello Sport)