DAR ES SALAAM: WINGA wa timu ya Simba, Ladack Chasambi amesema kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Kocha Fadlu Davids ni suala la muda tu.
Amesema kikubwa ni kuwa makini kama mchezaji na pale inapotokea hujapata nafasi haimaanishi kuwa wewe ni mchezaji mbaya bali ni wakati na wale wanaopata nafasi na muda wako utafika.
“Kupata nafasi kikosi cha kwanza ni suala la muda, ninapokosa nafasi hainiondoi mchezoni, nafanya mazoezi kwa bidii kusikiliza maagizo ya kocha, siku nikipata nafasi nifanye kile mwalimu anataka,” amesema.
Chasambi amesema hatakata tamaa haraka kwa sababu hapati namba kwenye kikosi cha kwanza na anaamini itafika muda wake atakuwa sehemu ya changuo la Fadlu.
Amesema anapopata nafasi anafuata maagizo ya kocha wake ambayo ili kuisadia timu kupata ushindi kama alivyofanya jana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola.