Ligi Kuu

Taoussi: Vijana wangu wana utulivu wa akili

KOCHA Mkuu wa Azam FC Rachid Taoussi, ameeleza anavyokoshwa na ari inayooneshwa na wachezaji wake kipindi hiki akisifu kuwa vijana wake wana utulivu wa akili.

Azam FC baada ya kutoka kushinda mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KenGold juzi tayari wametua Singida kwa ajili ya mchezo mwingine utakaochezwa kesho dhidi ya Singida Black Stars.

Taoussi amesema wachezaji wake wamekuwa wakionesha upambanaji uwanjani ndio maana imekuwa rahisi kupata matokeo mazuri akisema wanaendelea kusuka mpango kuendeleza ushindi.

“Wachezaji wangu wako vizuri, kila mchezaji amekuwa akionesha ubora wake. Tuna wachezaji wenye moyo wa kupambana, vijana wenye utulivu wa kimwili na kiakili uwanjani,”amesema.

Azam FC watakutana na Singida Black Stars ambao nao wamesema wanataka kulipiza kisasi baada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Msemaji wa Singida Black Stars Hussein Masanja amesema mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa CCM Liti ni muhimu kupambania matokeo mazuri na kuwahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.

Related Articles

Back to top button