AFCON

Taifa stars kuingia kambini leo

DAR ES SALAAM:TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaingia kambini leo jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi DR Congo.

Stars inatarajia kuondoka nchini jumatatu Oktoba 7 kwa ajili ya kuwavaa wapinzani hao na mechi ya kwanza itakuwa ugenini katika dimba la Des Martyrs, Oktoba 10, mwaka huu na Oktoba 15 watarudiana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kaimu Kocha Mkuu wa Stars, Hemed Morocco amesema wanatambua utakuwa mchezo mgumu na wanahitaji kupata matokeo mazuri katika mechi ya ugenini kujiweka katika mazingira mazuri katika kundi lao.

“Hautakuwa mchezo rahisi kila mmoja anahitaji kufanya vizuri na tumeita kikosi kulingana na tunavyowafahamu wapinzani wetu DR Congo aina ya mpira wanaocheza,” amesema Kocha huyo.

Tanzania ipo kundi H katika nafasi ya pili ikiwa na pointi nne iliyovuna katika michezo miwili ikiwa nyuma ya kinara DR Congo yenye pointi sita, Ethiopia nafasi ya tatu kwa pointi moja na Guinea ya mwisho haina pointi.

 

Related Articles

Back to top button