AfricaAfrika Mashariki
Tanzania U18 kutinga fainali CECAFA leo?
NUSU fainali za michuano ya ubingwa wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 zinazofanyika Kenya, Tanzania ikiwavaa wenyeji.
Katika nusu fainali nyingine Uganda itaikabili Rwanda, michezo yote ikifanyika uwanja wa Jomo Kenyatta uliopo mji wa Kisumu.
Kufika nusu fainali, Tanzania imeitoa Zanzibar kwa kanuni ya kadi chache za njano.